Dunia Bila Mawingu ni hadithi ya kufikiri na kubuni kuhusiana na wakati ujao. Hadithi hii inahusu wanaantropologia watano ambao wanajaribu kuokoa mawingu yaliyoko hatarini kutoweka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka ya 2045-50. Wanaantropologia watano hawa wakijiita “Wananefologia” (wao wanaochunguza mawingu). Wanavumbua mashine ya kuwasiliana na mawingu ili waweze kuyauliza mawingu, “Tutawaokoaje ninyi kabla hamjafa?” Mashine imehitimizwa kusikiliza mawingu haya maana mawingu yatawaambia Wananefologia njia ya kuyaokoa yao. Je, Wananefologia watafanikiwa kuokoa mawingu haya? Tunachanganya kuhadithia na taaluma ya usomi. Tungependa kutengeneza sehemu ya
'kupiga stori' kuhusu mambo ya kisayansi na kisomi. Tunauliza, Je, ni mfumo gani mpya wa mawingu utaweza kutokea wakati ujao? Tunakualika kushiriki katika hadithi hii.